Tuesday, June 28, 2011

Siku ya Wajane Duniani

Siku hii inaadhimishwa kwa mara ya kwanza duniani. June 23 imekuja kutokana na kampeni za mwanasiasa mmoja Muingereza ambae, alifiwa na baba yake akiwa mtoto nchini nchini India. Serikali ya Gabon ilidhamini azimio hilo la Umoja wa Mataifa.
Inakisiwa kuna takriban wajane millioni 245 duniani na 115millioni wanadhulumiwa wakikabiliwa na ukatili,umasikini na kutengwa na jamii.
Siku inayodhamira kutoa fursa ya kuzungumzia matatizo yanayowakumba wajane hasa wanawake na watoto wao ili kurejesha haki zao na kupambana na umaskini kwa kuwezeshwa.
Miongoni mwa matatizo yanayowakumba wajane ni pamoja na kunyimwa haki ya kurithi na haki ya kumiliki ardhi, na wengine hata hunyimwa haki ya kumzika mume wako.
Wajane hao wa kike wengine huondolewa kwenye nyumba zao na kupigwa, baadhi huuliwa na ndugu zao wenyewe.
Katika nchi nyingi, hadhi ya mwanamke inahusishwa zaidi na maisha yake na mumewe, na hivyo mume anapokufa, mwanamke anakuwa hana nafasi yeyote kwenye jamii.
Wengine hutakiwa kuolewa na ndugu wa mume wake bila ridhaa zao. Na huo ni mwanzo tu wa matatizo mengi yajayo.
Watoto wa wajane hao nao huathirika sana kisaikolojia na kiuchumi.
Wajane wengine hulazimika kuwatoa watoto wao shuleni, ukizingatia hana msaada wowote hivyo watoto kufanya kazi za kuinua maisha yao.
Wachangiaji katika mjadala huu ni
Bi Tuzie Muze- mjane aliyopo Dar es Salaam, Tanzania.
Bi Rosemary Nafula- mjane aliyopo Kenya
Bi Jane Magigita- mwanasheria kutoka kituo cha msaada wa sheria kwa wanawake, WILAC- Dar es Salaam
Judy Okal- wakili kutoka shirikisho la wanawake wanasheria nchini Kenya

Ocean View yaingia robo Fainali

Timu ya Zanzibar Ocean View imekuwa ya kwanza kujihakikishia kuingia hatua ya Robo fainali katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama kombe la Kagame baada ya kushinda mechi ya pili mfululizo kwa kuichapa Red Sea ya Eritrea 2-0 katika mchezouliocheza kwenye uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, Tanzania.
Cecafa
Kombe la Kagame


Katika mchezo wa kwanza ulichezwa siku ya ufunguzi wa michuano hiyo Jumamosi Zanzibar Ocean View waliilaza Etincelles ya Rwanda 3-2.

Wakiwa wenye kujiamini Zanzibar Ocean View walipata goli la kwanza katika dakika ya 35 kipindi cha kwanza goli lililofungwa na Suleiman Haji kwa shuti kali baada kupokea pasi kutoka kwa Mohamed Hamduni hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Zanzibar Ocen View ilitoka kifua mbele kwa 1-0.

Kipindi cha pili kilikuwa cha mshikemshike lakini ni Zanzibar Ocean View walioonekana kuutawala zaidi mchezo huo ambapo katika dakika ya 86 Said Rashid alimalizia karamu ya leo kwa kufunga goli la pili hadi mpira unamalizika matokeo yalikuwa 2-0.

Katika mchezo huo Aron Zakarias wa Red Sea alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia faulo mbaya Salum Shebe wa Zanzibar Ocean View.

Katika mchezo wa pili timu ya Vital’o FC ya Burundi imejiweka katika mazingira mazuri ya kuingia hatua ya Robo Fainali baada ya kuifunga timu ya Entincelles ya Rwanda kwa magoli 3-1.

Katika mchezo wa awali timu hiyo ya Vital’o FC ilitoka sare ya kutofungana na timu ya Simba ya Tanzania.

Magoli ya Vital’o FC yamefungwa na Steive Nzigamasabo, Stanley Minzi na Miami Mbakiye huku goli pekee la Entincelles likifungwa na Claver Muhire

Kwa matokeo hayo timu ya Zanzibar Ocean View ndio wanaoongoza kundi A wakiwa na jumla ya pointi 6 baada ya kushinda mechi zote mbili huku Vital’o ya Burundi ikishika nafasi ya pili ikiwa na pointi 4.
Timu ya Simba ya Tanzania ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi moja wakati timu za Entincelles ya Rwanda na Red Sea ya Eritrea hazina pointi.

Barabara ya vumbi tosha Serengeti

Mipango iliyojaa utata ya kujenga barabara ya lami katikati ya mbuga ya wanyama ya Serengeti na sasa baada ya ubishi na kuonywa kuwa mpango huo utaathiri mazingira na nyenzo za wanyama pori.
Ajabu ya dunia Serengeti
Thamani ya mazingira ni kubwa

Serikali ya Tanzania ilipanga barabara mbili yaani ya kutoka na inayoelekea kupitia mbuga hiyo kutoka ukingo wa Ziwa Victoria na pwani.
Lakini utafiti uliofanywa umeonyesha kuwa mpango huo utaathiri vikali hali ya wanyama kama vile nyumbu na punda milia, ambao misafara yao ya kuhama, jambo ambalo linaangaliwa kama maajabu ya maumbile Duniani.
Serikali sasa imethibitisha kuwa barabara hiyo haitoguswa na itabaki kuwa ya vumbi.
Katika barua kwa Kituo kinachoshughulikia Hifadhi ya Mazingira Duniani mjini Paris, Idara ya mali asili na Utalii nchini Tanzania imesema kuwa sehemu ya barabara hiyo yenye umbali wa kilomita 50 itaendelea kusimamiwa kwa ajili tu ya utalii na utawala.
Serikali kwa sasa inatathmini njia nyingine ingawa itakuwa ndefu kuweza kuwafikishia wananchi wake huduma kupitia kusini mwa mbuga hiyo ya wanyama.
Barabara hiyo itaepuka maeneo yenye thamani ya kuhifadhi mazingira na athari zinazoweza kufuata.
Nyumbu wa Serengeti
Serengeti

Mwaka jana, kundi la wataalamu walionya kua barabara iliyopendekezwa kupitia mbuga ya wanyama inaweza kupunguza idadi ya Nyumbu wanaokadiriwa kuwa milioni 1.3 kufikia 300,000.
Athari kwa wanyama pori, wataalamu hao walionya kuwa Uchumi utaathirika mno kutokana na kupungua kwa wanyama hao.
Wataalamu hao waliitaja mbuga ya wanyama ya Serengeti kama mfano wa kipekee wa hifadhi ya wanyama wanaohamahama.
Safari ya kuhama hama kwa wanyama hao kila mwaka hushiriki takriban wanyama milioni 1.5, wakiwemo nyumbu na punda milia.
Wakati wanyama hao wakisafiri, huacha vinyesi ardhini, ambavyo husaidia kurutubisha mimea, huku nyayo zao zikizuwia ukuaji wa kupindukia wa nyasi.
Mabadiliko ya aina yoyote katika hali kama hiyo, wataalamu hao wamesema kwenye ripoti yao kwa serikali ya Tanzania, yatasababisha kupungua kwa wanyama wanaotegemea nyumbu na punda milia kama chakula chao kama simba,chui na duma.
Simba watatoweka
Simba

Hawa ni baadhi ya wanyama wanaovutia mno watalii.
Halikdhalika wataalamu hao wameonya kuwa barabara hiyo ingeweza kusababisha kubadilika kwa mimea na vilevile kusafirisha aina mbalimbali za magonjwa yasiyokuemo ndani ya mbuga.

CRDB bank sets its sights on EAC untapped market

 
CRDB managing director, Dr Charles Kimei
The CRDB bank is set to expand its banking services in the East African countries, in an effort to exploit the untapped regional market.
CRDB managing director, Dr Charles Kimei revealed this here over the weekend when speaking at the one-day seminar which involved more than 100 shareholders of the bank.
He said that the bank’s idea is meant to empower East Africans economically and use the bank as a ladder to prosperity.
If the mission will be fulfilled, CRDB bank will be the first Tanzanian bank to explore the untapped potentials available in the EAC. In another development, Dr Kimei stated that the Dar es Salaam Stock Exchange has not been well exploited by Tanzanians due to the limited number of brokers in the newly established capital market.
He cited other factors as limited knowledge on the significance of the Dar bourse to boost the country’s economic prosperity.
“After realising that we have already embarked on a programme to educate our shareholders on the significance of the DSE market, of which if well utilised it will help to transform people’s lives,” he told the fully packed gathering.
He added: “The only thing people know, is for them to buy shares…but in reality there are more than that.”
Dr Kimei explained that his bank uses special brokers in selling and buying shares contrary to the previous system whereby a shareholder was forced to buy shares in the bank’s branch or through the DSE of which the bank is a member since 2009.
“Currently, there are limited number of brokers enabling people to participate in the bourse market, because we have learnt there are over 200,000 Tanzanians who have shares at the DSE, which is a very small number. That is why we deployed special brokers who will be providing services in all of our branches across the country,” he said.
The bank’s senior official noted that there are many areas which have no such services, hence the new initiative to enable the bank’s customers easily buy and sell their shares.
He explained that there is a need for Tanzanians to understand issues related to shares and its technicalities.
One of the bank’s shareholders, Esterina Tarimo from Moshi municipality in Kilimanjaro region stressed the need for shareholders to understand the key issues related to shares.

Z`bar Ocean View cruise into Kagame Cup quarterfinals

Ocean View FC squad that became the first side to reach the Kagame Cup last eight.
Zanzibar Ocean View became the first out of the 13 teams competing in this year’s Kagame Cup to cruise into the last eight following their resounding 2-0 victory over Eritrea’s Red Sea at the national Stadium in Dar es Salaam yesterday.
The former Zanzibar champions who are making their debut appearance in the regional championship have so far collected six points to top group A courtesy of wining the Saturday’s opener against Rwanda’s Etincelles.
Suleiman Haji scored the Zanzibar Ocean View opener after 35 minutes when he connected home Mohamed Hamduni’s cross.
Said Rashid wrapped up the business for the Zanzibar side with a power packed shot that sailed into the net.
The former Zanzibar champions have so far collected four points to stay on course for the quarterfinal progression with two matches in hand.
This is a milestone achievement for the side that is making a debut appearance in the championship after finishing runners up in the premiership.
The Zanzibar side meets Simba at the same venue tomorrow as they play with a great composure after sealing of the last eight stages yesterday.
The team has wide options of choosing their next opponents in the quarters through winning or drawing their remaining matches.
Tanzania has fielded three teams in the tourney including Yanga and Simba for the Mainland.
Dk Mathayo aagiza Narco ianze kunenepesha ng’ombe  Send to a friend
Monday, 27 June 2011 20:32

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dk David Mathayo
Festo Polea, Kongwa
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Dk David Mathayo, ameagiza Shirika la Ranchi za Taifa (Narco) kuanzisha kitengo cha mafunzo ya unenepeshaji mifugo kwa wafugaji, ili kuwa na mifugo yenye tija kwenye soko la nje.
Dk Mathayo alisema hayo juzi alipokuwa akizindua duka la nyama la Kongwa lililopo ranchi ya Kongwa, Wilaya ya Kongwa nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Alisema licha ya Tanzania kuwa ya tatu kwa idadi kubwa ya ng'ombe barani Afrika baada ya Sudani na Ethiopia, inauza tani 200 za ng'ombe kati ya milioni 20.
"Haiwezekani tuwe na ng'ombe wengi kiasi hicho, halafu tuuze tani 200 tu, idadi ambayo ni ndogo na haibu kuitaja kwa watu, hivyo naagiza kuanzishwa kwa kituo cha kutoa mafunzo jinsi ya kunenepesha mifugo ili tuweze kupata soko kubwa la nje ambalo litatusaidia kunyanyuka,” alisema Dk Mathayo.
Alishauri Narco kuomba mikopo kutoka benki nchini kuwekeza katika unenepeshaji mifugo hiyo, ili kufikia lengo walilojiwekea la kuuza idadi kubwa ya mifugo nchi za nje.
Katika hatua nyingine, Dk Mathayo aliwataka wafugaji wadogo  nchini kufuga mifugo kulingana na ukubwa wa maeneo wanayomiliki.
Naye Meneja Mkuu wa Narco, Dk John Mbogoma, aliomba serikali kusaidia changamoto zinazolikumba shirika hilo zikiwamo kutoa ufumbuzi wa uvamizi wa mara kwa mara wa maeneo ya ranchi.
Mwisho.
BOOKMARK THIS PAGE
Mbunge ailipua Ikulu,  Send to a friend
Monday, 27 June 2011 21:00
0diggsdigg

Jengo la Ikulu jijini Dar es Salaam
Kizitto Noya, Dodoma
MBUNGE wa Chadema, Suzan Lyimo ameishangaa Serikali kwa kutenga mabilioni ya fedha kwa ajili ya ukarabati wa Ikulu ya Dar es Salaam kila mwaka, huku Serikali hiyo hiyo ikiendelea kusisitiza mikakati ya kuhamia Dodoma.
Akichangia mjadala wa bajeti kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na ofisi zilizopo chini yake, kwa mwaka wa Fedha 2011/12 jana, Lyimo alisema haungi mkono hoja hiyo, mpaka apewe majibu ya kuridhisha ya sababu za Rais kushindwa kuhamia Dodoma na badala yake kuendelea kutenga kiasi kikubwa cha fedha kukarabati Ikulu ya Dar es Salaam.

Akitoa takwimu mbalimbali za bajeti ya Ikulu tangu mwaka 2001 hadi mwaka 2011, Lyimo alisema kwa kipindi hicho cha miaka kumi, Ikulu imekwishatengewa zaidi ya Sh50 bilioni, fedha ambayo kwa maoni yake, zinatumika vibaya.

"Siungi mkono hoja hii kwa sababu tatu; moja ni ukubwa wa Baraza la Mawaziri, mbili uonevu  wanaofanyiwa wanafunzi wa elimu ya juu na tatu Serikali kutokuwa na mpango wa dhati wa kuhamia Dodoma," alisema Lyimo alipoanza kuchangia mjadala huo.

Kwa mujibu wa mbunge huyo wa Viti Maalumu, kitendo cha Serikali kuendelea kuliomba Bunge liidhinishe matumizi ya Sh10 bilioni kwa ajili ya ukarabati wa Ikulu ya Dar es Salaam katika kipindi cha mwaka 2011/2012, kinaonyesha kuwa haina nia ya dhati wala utashi wa kisiasa kutekeleza mpango wa kuhamia Dodoma.

"Tangu mwaka 2001 hadi 2011, Ikulu hiyo imetengewa Jumla ya Sh56 bilioni. Kila mwaka Serikali inaomba Sh2 bilioni, mwaka jana iliomba Sh7.2 bilioni na mwaka huu imeomba Sh10 bilioni," alilalamika Lyimo na kuendelea:

"Hivi ni kweli mabilioni hayo yanatengeneza Ikulu ya Rais tu pale Dar es Salaam? Na kama kweli ni Ikulu, kwa nini isitengenezwe Ikulu ya Chamwino ili Rais ahamie Dodoma?" alihoji

Lyimo alisema haoni mantiki kwa Rais kuendelea kuishi Dar es Salaam wakati mpango wa kuhamia Dodoma ulianza tangu mwaka 1976 na kila mara Serikali imekuwa ikiendelea kusisitiza mpango huo.

"Mheshimiwa mmoja hapa alipendekeza Spika ahamie Dodoma, mimi nasema sio Spika ni Rais ndiye anayepaswa kuja Dodoma. Na kama Rais anahamia Dodoma hakuna waziri atakayebaki Dar es Salaam. Tunamtaka pia Waziri Mkuu kuja Dodoma," alisema.

Baraza ni mzigo
Kuhusu Baraza la Mawaziri, Lyimo alisema ni kubwa kupita kiasi na kwamba Serikali inapaswa kulipunguza ili kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima serikalini.

Alisema mawaziri 54 waliopo sasa, ni wengi mno na wanaiongezea mzigo wananchi ambao ndio wanaobeba jukumu la kuigharimia Serikali yao.

"Baraza la Mawaziri ni kubwa mno, wako 54 ukimjulisha na Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Rais wa Zanzibar. Nchi tajiri kama Marekani ina mawaziri 15 tu, kwa nini Tanzania ambayo ni maskini iwe na mawaziri wote hao?" alihoji na kusisitiza, "tunaomba Serikali iliangalie upya baraza lake la mawaziri."

Katika hoja ya uonevu aliodai unafanywa na Serikali kwa wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu, Lyimo alihoji sababu za wanafunzi kufukuzwa baada ya kufanya  migomo na maandamano wakati kisheria, inaruhusiwa vyuoni.

Muungano watikisa
Katika hatua nyingine, hoja ya Muungano jana ilitawala mjadala huo unaoendelea bungeni baada ya wabunge kadhaa kutoka Zanzibar, kueleza kuwa bado una kero nyingi na hivyo kupendekeza uvunjwe.

Wakichangia mjadala huo kwa nyakati tofauti, wabunge hao walisema Muungano bado ni kero kwa Wazanzibari kwa kuwa kuna mambo mengi ya msingi ambayo yanatendeka bila kujali maslahi ya pande zote mbili.

Mbunge wa Mgogoni, Kombo Khamis Kombo alihoji namna haki inavyoweza kutendeka katika mazingira ya nchi hizi mbili kuungana kwenye wizara sita tu kati ya wizara 26 zinazounda Serikali ya Muungano.

"Seriklai hii ina wizara 26 na wizara za Muungano ni sita tu. Mambo yote yanayofanywa kwenye wizara ambazo sio za Muungano bajeti yake inapangwa na kutekelezwa na Serikali ya Muungano, sasa licha ya jambo hilo kuwa kikatiba, kutakuwa na usawa gani kati ya Zanzibar na Tanganyika?" alihoji.

Mbunge huyo alisema haamini kama Serikali ya Muungano ina nia ya dhati katika kutatua kero za muungano na kama ina nia ya kweli, iwajengee imani Wazanzibari kwa Waziri Mkuu kuzungumzia kero hizo wakati anajibu hoja za wabunge katika mjadala unaoendelea.

"Mheshimiwa Spika, katika mazingira haya, tunawahakikishia Wazanzibari kuamini kuwa Tanganyika (Tanzania Bara) inawadhalilisha. Zanzibar kuna mabalozi wanne tu tena wanapelekwa kwenye nchi za Kiarabu na sasa China amepaelekwa mheshimiwa Mapuri. Wazanzibari wana haki, uwezo na haki ya kupeleka wafanyakazi katika balozi,"alieleza.

Kombo alisema kitendo cha Serikali kupuuza mapendekezo ya kamati ya Nyalali, Shelukindo na Amina Salum Ally kuhusu kero za Muungano ni ishara tosha kwamba haina nia ya dhati kutatua kero hizo zinazolalamikiwa na Wazanzibari.

Maelezo hayo yaliungwa mkono na mbunge wa Micheweni (CUF), Haji Khamis Khai aliyeeleza kuwa Wazanzibari hawana imani na Muungano huo kwa kuwa wao ni maskini kuliko Tanzania Bara.

"Kama Zanzibari ni mzigo kwenu (Bara) tuvunje muungano huo, mtuache," alisema.

Alisema inaudhi Wazanzibari kuzungumzia kero za Muungao kila siku na Serikali ya Muungnao ikiendelea kuwa kimya bila kutoa kauli inayotekelezeka."Tunaomba Muungano uvunjwe na uundwe tena kama ni lazima," alisema.

Hii ni mara ya pili kwa wabunge kujadili hoja ya Muungano katika Mkutano huu wa nne unaondelea sasa. Mara ya kwanza hoja hiyo iliibuliwia na mbunge wa Chwaka (CCM), Yahya Kassim Issa ambaye aliliambia Bunge kwamba  Muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar, bado una sintofahamu nyingi.

Akichangia Hotuba ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda Kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Matumizi ya Fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Bunge ya mwaka 2011/2012 jana, mbunge huyo alisema suala la Muungano bado lina utata unaopashwa kushughulikiwa haraka.

"Mheshimiwa Spika, Wakati Rais akitolea ufafanuzi suala hilo la Muungano alieleza kuwa Zanzibar ni nchi ndani ya nchi ya Tanzania lakini, Nje ya nchi, nchi ni Tanzania. Lakini mheshimiwa spika, mpaka leo vitabu hivi, bado vinaitambua Zanzibar kuwa ni mkoa kama ulivyo Kilimanjaro!"

"Mbona vitabu havitoki kubadilisha hilo ili Zanzibar isomeke kuwa ni nchi kama Rais alivyosema? Huu ni mzozo, Zanzibar kuonekana kama mkoa na sisi (Wazanzibari), hatutaki," alilalamika.